Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea wamtandika mtu bao 5 EPL

IMG 6878.jpeg Wachezaji wa Chelsea wakishangilia

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji Chelsea wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Waingereza viungo Cole Palmer dakika ya 15, Conor Gallagher dakika ya 30, washambuliaji Chukwunonso Madueke dakika ya 36 na Msenegal Nicolas Jackson dakika ya 48 na 80.

Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 35 na kusogea nafasi ya saba, wakati West Ham United inabaki na pointi zake 49 za mechi 36 sasa nafasi ya tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live