Chelsea walijitutumua na kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wao wa pili wa raundi ya 16 bora ya Ligi Mabingwa Ulaya na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund.
Ushindi huo umempa ahueni Graham Potter kutokana na presha kubwa iliyotawala ndani ya viunga vya Stamford Bridge kwasababu timu ilikuwa haipati matokeo mazuri.
Sasa timu vijana wa Potter wametinga robo fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya na wanachosubiri ni droo ya hatua hiyo inayofuata ambayo itapangwa Ijumaa ijayo.
Haya ndio mabao matano yaliochangia Chelsea kung'ara usiku wa Ligi Mabingwa Ulaya
1. Kai Havertz Nyota huyu alicheza kwa kiwango kikubwa akisimama kama straika eneo la hatari. Muda wote wa mchezo alikuwa anamiliki mipira licha Dortmund kukomaa.
2. Marc Cucurella
Beki huyo aliwapondwa sana na mashabiki wa Chelsea baada ya kuboronga hivi karibuni licha ya kununuliwa kwa kitita cha Pauni 65 milioni akitokea Brighton.
Lakini katika mchezo dhidi ya Dortmund alikuwa moto wa kuotea mbali akitokea upande wa kushoto. Cucurella alipewa tuzo ya mchezaji aliynga'ara kwenye mechi hiyo ya mtoano.
3.Sehemu Kiungo
Safu ya kiungo ya Chelsea iliyoundwa na Enzo Fernandez pamoja na Matteo Kovacic ilivuruga safu ya kiungo ya Dortmund akiwemo Jude Bellingham.
4. Ben Chilwell
Alicheza vizuri upande wa kulia akishirikiana na Cucurella. Dakika zote za mchezo mipira yake ilikuwa hatari.
5.Kepa mikono mia
Kepa Arrizabalaga aliokoa michomo mitatu na kuisaidia Chelsea kuepuka kichapo dhidi ya Dortmund, vile vile alikuwa akirusha mipira mirefu mbele kila mara kwenye mechi kama sehemu ya kujilinda.