Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea wachezea kichapo kikali EPL

Chelsea Beaten By Brighton Brighton waliibuka na ushindi wa mabao 4-1

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Brighton & Hove Albion jana waliiadhibu Chelsea kwa kuitandika mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Amex,

Mabao ya Brighton yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya tano, kabla ya wachezaji wawili wa Chelsea kujifunga Ruben Loftus-Cheek dakika ya 14 na Trevoh Chalobah dakika ya 42, huku bao la nne la wenyeji likifungwa Pascal Gross dakika ya 90 na ushei, wakati la kufutia machozi la The Blues lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 48.

Kwa matokeo hayom, Brighton inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nane, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 21 katika nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live