Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea wachapika Stamford Bridge

IMG 8759.jpeg Chelsea wachapika Stamford Bridge

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji Mbrazil, Matheus Cunha amefunga mabao matatu kuiwezesha Wolverhampton Wanderers kuichapa Chelsea 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumapili Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

Cunha amefunga mabao hayo dakika za 22, 63 na 82, wakati bao lingine la Wolves limefungwa na beki Mfaransa, Axel Disasi aliyejifunga dakika ya 43, wakati mabao ya Chelsea yamefungwa na Cole Palmer dakika ya 19 na Thiago Silva dakika ya 86.

Kwa ushindi huo, Wolves inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya 10, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 31 na inashukia nafasi ya 11, baada ya wote kucheza mechi 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live