Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea waandaa mkwanja mrefu kumnyakua Nunez Liverpool

Nunez Chelseaaaaaaa Darwin Nunez

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea imeandaa kitita cha pauni 84 Million kunasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Darwin Nunes kama sehemu ya kuongeza nguvu eneo lake la ushambuliaji ambalo kwa sasa linaongozwa na Nicolas Jackson na Christopher Nkunku.

Hata hivyo Liverpool chini ya Jurgen Klopp haipo tayari kumuuza nyota huyo kwasasa ambaye amekuwa kwenye kiwango bora sana.Nunez alikosekana kwenye mchezo wa jana wa fainali ya Carabao dhidi ya Chelsea.

Hata hivyo licha ya kukosekana hapo jana, Liverpool ilibeba kombe hilo na nyota huyo anatarajiwa kukosekana tena kwenye mchezo wa jumatano dhidi ya Southampton utakaopigwa saa 5 Usiku.

Wakati Liverpool anajitetea kutafuta kombe lingine la pili msimu huu, Manchester City nae anatengeneza njia ya kupata kombe la kwanza la FA dhidi ya Luton jumanne hii majira ya saa tano [23:00] usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live