Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea pumzi imekata, yalazimishwa sare darajani

Chelsea Everton Kiungo wa Chelsea, Jorginho akiwa haamini matokeo waliyoyapata

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chelsea imeendelea kuangusha tena pointi baada ya kulazimishwa sare nyumbani ya bao 1-1 na vijana wa kocha Rafael Benitez, Everton, mtanange uliopigwa dimba la Stamford Bridge huku mabao yote mawili yakifungwa katika utofauti wa dakila nne pekee za kipindi cha pili.

Bao la Chelsea limefungwa na kiungo mshambuliaji Mason Mount kunako dakika ya 70 akimalizia krosi wa beki wa kulia Reece James wakati bao la Everton likitupiwa na Jarrad Branthwaite.

Beki Thiago Silva alikuwa na nafasi ya kuipa Chelsea ushindi lakini nafasi hiyo akaipoteza huku kipa Pickford akiwa kikwazo kikubwa.

“Kushinda mchezo muda mwingine unahitaji kuwa na zaidi ya bahati, lakini sisi hatuna hiyo bahati”, alisema kocha wa Everton Rafael Benitez.

The Blues wanafikisha pointi 37 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa EPL wakati Everton ambayo imekuwa na kiwango cha chini juu inakamata nafasi ya 14 na alama 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live