Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea kuvuta mkwanja FIFA

Chelsea To Army.jpeg Chelsea FC

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea itapewa kitita cha Pauni 50 milioni baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuthibitisha timu hiyo imefuzu michuano mipya ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu.

Mkutano wa viongozi wakuu uliyofanyika Rwanda ulikubaliana muundo mpya wa kufuzu michuano hiyo ambao utashirikisha timu 32 utaanza kufanyika 2025 nchini China.

Ulaya imepewa nafasi kubwa zaidi ikiwa na timu 12, huku Fifa ikikubali kuwa timu zilizofuzu ni ndani ya kipindi cha miaka minne kuanzia misimu ya 2020-21 hadi 2023-24.

Inamaanisha kuwa washindi wanne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika misimu hiyo pamoja na timu nane zinazofuata kwenye mfumo wa viwango vya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), zitapata nafasi ya kushiriki mashindano hayo mapya yenye mkwanja mrefu kwa mshindi ambaye atafanikiwa kufuzu na kushinda ubingwa.

Chelsea imepata nafasi ya kufuzu kwa sababu ilibeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2021 chini ya kocha Thomas Tuchel, na sasa vijana wa kocha Graham Potter wanaungana na Real Madrid ambayo ilibeba msimu uliopita.

Hakuna nchi ambayo itachukua zaidi ya nafasi mbili za ushiriki, lakini mpaka sasa kwa mujibu wa mchanganuo huo, Liverpool na Manchester City zimeonekana kufuzu michuano hiyo.

Hata hivyo, endapo Liverpool itakosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao itafungua milango kwa Manchester United kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa.

Fifa pia itarekebisha kidogo kanuni za michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya klabu ambayo imepangwa kufanyika kila mwaka. Mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ataingia fainali moja kwa moja.

Chanzo: Mwanaspoti