Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea kumvuta Ronaldo

Ronaldo 1140x640 Chelsea kumvuta Ronaldo

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea inaripotiwa huenda ikabadili msimamo wake na kufanya usajili wa nyota wa Manchester United na moja yaw achezaji bora wa muda wote wa mpira wa miguu duniani, Cristiano Ronaldo endapo tu Manchester United itamvunjia mkataba mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Mirror, limeripoti kuwa Manchester United wapo katika hatrua za awali za kuvunja mklataba wa nyota huyo na kuwafanya Chelsea kufikiria uwezekano wa kumchukua nyota huyo katika kipindi cha dirisha dogo la mwezi Januari.

Ronaldo amepitia kipindi kigumu ndani ya kikosi hicho cha Manchester United chini ya kocha mpya Erik Ten Haag hali iliyosababisha kuikosoa vikali klabu hiyo kwenye mahojiano maalum aliyofanya na mwandishi wa Habari Piers Morgan.

Kwa sasa nyota huyo yupo na kikosi cha Ureno kinachoshiriki Mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, na kwa mujibu wa ripoti kutoka vyanzo mbalimbali vya Habari za michezo barani Ulaya ni kuwa mpango wa Manchester United ni kutomruhusu Ronaldo kurudi katika viunga vya Carringthon mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live