Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea kukutana na Bayern au Real Madrid 16 bora?

0 GettyImages 1341475636 Chelsea huenda wakakutana na Vigogo hatua ya 16 bora UEFA

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Droo ya mtoana ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajia kufanyika siku ya Jumatatu December 13, baada ya timu 16 kufuzu kwaajili ya hatua hiyo inayotarajia kutimua vumbia mwakani 2022, mwezi wa pili.

Timu zilizofuzu hatua ya 16 bora ni, Real Madrid, Atletico Madrid, Manchester City, Liverpool, Ajax, Bayern Munich, Manchester United, Lille, Juventus, Paris Saint-Germain, Sporting CP, Inter, Benfica, RB Salzburg, Chelsea and Villarreal.

Katika hatua hii timu kutoka nchi moja haziwezi kukutana, vilabu vilivyocheza katika kundi moja pia navyo haviwezi kuchuana katika hatua hii sanjari ya yote timu zilizomaliza na nafasi ya kwanza zitaanza ugenini huku timu zilizomaliza nafasi ya pili zikianza nyumbani.

Mabingwa watetezi wa kombe Champions League, Chelsea The Blues wanakibarua kizito kuelekea siku ya Jumatatu ya December 13, kwakuwa kuna asilimia 75% ya kukutana na Bayern Munich, Real Madrid na Ajax.

Chanzo: eatv.tv