Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea kukatwa Pointi EPL

IMG 6157.jpeg Majanga Chelsea

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea inaweza ikapunguziwa pointi baada ya Ligi ya England kuanza uchunguzi rasmi kuhusiana na uhamisho wa Willian na Samuel Eto’o.

Wachezaji hao walisainiwa wakati wa utawala wa Roman Abramovich wakitokea klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Inadaiwa kuwa kuna malipo yalifanywa kwa mashirika ya Urusi ambayo ni pembeni kabisa ya ada ya uhamisho. Vilevile malipo kwa familia ya mchezaji mmojawapo yanachunguzwa.

Mwezi Agosti, Ligi ya England ilianza rasmi uchunguzi juu ya masuala yote ya kifedha wakati wa utawala wa Abramovich ikiwemo uhamisho wa wachezaji.

Klabu hiyo imesema ”madai haya ni ya zamani, na mashirika yaliyopokea pesa yanadaiwa kuwa chini ya mmiliki wa zamani wa klabu hii, na hayana uhusiano wowote na wamiliki wa sasa”.

Taarifa zinadai kuwa wamiliki wa sasa wa Chelsea ndio walioibua kashfa hiyo baada ya mchakato uliofanyiwa mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live