Klabu ya Chelsea ina nafasi kubwa ya kuirahisishia kazi Liverpool ya kukwea juu ya Arsenal kwenye msimamo wa Ligi kuu kandanda England.
Chelsea iliyopo nafasi ya 9 itashuka dimbani kesho saa nne (22:00) usiku kuikabili Arsenal ambayo ni kinara kwenye msimamo ikiwa na alama 74 sawa na Liverpool katika nafasi ya pili.
Kama Chelsea itashinda, basi Liverpool italazimika pia ishinde kwenye mchezo wake wa Jumatano dhidi ya Everton utakaopigwa saa nne (22:00) usiku ili ipande juu ya msimamo.
Wakati wakijizungusha kwenye eneo hilo la juu la msimamo mwenye nafasi yake Manchester City ipo nafasi ya tatu na alama 73 ikiwa imecheza michezo 32, mchezo mmoja pungufu kwa Liverpool na Arsenal.
Kitu cha kufurahisha zaidi kwa Chelsea kama wakishinda mchezo huo wataiondoa Manchester United kwenye nafasi ya saba (7) na itashuka hadi nafasi ya nane [8].