Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea kuifanyizia Manchester United

Michael Akpovie Olise Winga wa Crystal Palace na Ufaransa, Michael Olise

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Chelsea imejitosa katika dili la kumuwania kiungo mshambuliaji wa Crystal Palace, Michael Olise, katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Chelsea imedhamiria kuipata saini ya kiungo huyo, huku ikimweka karika orodha kuu ya wachezaji wanaotakiwa kutua Stamford Bridge na kufanya kazi na Kocha mpya, Enzo Maresca.

Hata hivyo, The Blues huenda ikapata upinzani kutoka kwa Manchester United, ambayo pia imemweka kwenye orodha ya wachezaji inaotaka watue Old Trafford msimu ujao.

Olise alikuwa mchezaji bora wa Crystal Palace msimu uliopita, akifunga mabao 10 na asisti sita.

Kikosi cha Erik ten Hag kwa muda mrefu kimekuwa kikihusishwa na usajili wa kiungo huyo mzaliwa wa England, lakini amechagua kuitumikia Ufaransa kimataifa.

Gazeti la Mail linaeleza Chelsea imejizatiti kuipata saini ya Olise kwa gharama yoyote, ikiwa ni sehemu ya kuboresha kikosi chao, baada ya kufanya vibaya msimu uliopita.

"Chelsea inaendelea kufuatilia maendeleo ya Olise kwa karibu na sasa inafikiriwa kuwa tayari kufufua nia yao kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22," imeeleza ripoti ya Gazeti la Mail.

"Nyota huyo wa zamani wa akademi ya Chelsea anatajwa kuwa na furaha huko Selhurst, huku akipendezwa na uwezo wa kikosi chao chini ya Kocha Mpya Oliver Glasner.

"Olise angependelea kucheza Michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao, pia anaweza kuondoka endapo Palace itapata ofa nzuri.

"The Blues itahitaji kumtumia kocha wao mpya Maresca ili kufanikisha ushawishi wa kumsajili Olise.”

Chanzo: Mwanaspoti