Klabu ya Chelsea imetangaza itafuturisha kwenye uwanja wake wa Stamford Bridge, Jumapili ya Machi 26 katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Chelsea itaingia kwenye historia kwa kuwa klabu ya kwanza England kufanya hivyo ambapo itaandaa futari na kuwafuturisha waislamu ambao watakuwa kwenye funga ambayo inatarajiwa kuanza Jumatano ya Machi 22 hadi Ijumaa Aprili 21.
Futari hiyo itaendeshwa kwa ushirikiano na Mradi wa Ramadan Tent Project, shirika la usaidizi lililoanzishwa mwaka 2013 kwa dhamira ya kuleta jamii pamoja na kukuza uelewa wa Ramadhani.
Ramadan Tent Project, ambao mwaka huu wanasherehekea kumbukumbu ya miaka 10, huandaa Tamasha la kila mwaka la Ramadhani ambalo ni sherehe ya kila mwaka ya sanaa, utamaduni na ubunifu inayohamasishwa na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hivyo wafanyakazi wa Chelsea watajumuika na watu mbalimbali kwa ajili ya kufuturu.
Omar Salha, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Hema la Ramadhani, alisema: 'Kwa muongo mmoja uliopita Mradi wa Hema la Ramadhani umeunganisha na kuwakutanisha zaidi ya watu nusu milioni kutoka kila aina kupitia Tamasha lake la kila mwaka la Ramadhani na mpango mkuu wa Open Iftar.
‘Tuna heshima ya kuleta Open Iftar Stamford Bridge, katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 na mada yetu ya 2023 ya “Belonging”, na kufanya kazi kwa ushirikiano na Chelsea FC ambao wamekuwa wakiendesha ushirikishwaji wa soka. Kwa kiwango kama hicho, "Pride of London" itakuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu England katika historia kuandaa tukio la Open Iftar.
Mwezi huu wa Ramadhani unatambuliwa na Chelsea FC na Chelsea Foundation kama sehemu ya kampeni ya No To Hate, ambayo ni programu ya usawa, utofauti na ushirikishwaji wa klabu ambayo inalenga kuondoa chuki na ubaguzi kwa kuelimisha wadau wote ndani na nje ya Chelsea FC na soka