Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea kibishi yailaza Watford 2-1 Vicarage Road

NewFile 4 Chelsea wakishangilia goli la ushindi lililofungwa na Ziyech

Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara kunako EPL, Chelsea jana wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vicarage Road mjini Watford.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dakika ya 29 na Hakim Ziyech dakika ya 72, wakati la Watford lilifungwa na Emmanuel Dennis 43.

Chelsea inafikisha pointi 33 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya Manchester City na mbili zaidi ya Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 14, wakati Watford inabaki na pointi zake 13 za mechi 14 nafasi ya 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live