Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea inashuka daraja, Man United haimo Top 4

Chelsea 2023 24 Chelsea inashuka daraja, Man United haimo Top 4

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Aston Villa ya Unai Emery imekuwa moja kati ya timu zilizofanya vyema kwelikweli kwenye Ligi Kuu England kwa matokeo ya ndani ya mwaka huu wa 2023.

Kwa matokeo hayo ya mechi za Ligi Kuu England kwa mwaka huu, Liverpool imekuwa na rekodi nzuri kuizidi Manchester United, huku Brighton ikikusanya pointi nyingi kuliko Newcastle United na Nottingham Forest imekuwa na mambo matamu ndani ya uwanja kuliko Chelsea.

Man United ya Erik ten Hag imeibwaga Liverpool kwenye Top Four ya Ligi Kuu England msimu uliopita na kunyakua tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, lakini kama hesabu zingefanywa kwa kuzingatia mechi za mwaka huu pekee, kikosi hicho cha Jurgen Klopp kisingezidiwa na Man United.

Liverpool imekuwa na kiwango bora sana kwenye Ligi Kuu England kwa mwaka huu ikivuna pointi za kutosha na kushika namba nne kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa mwaka huu 2023.

Chama la Pep Guardiola, Manchester City limezidi kuthibitisha kwanini lilinyakua ubingwa huo baada ya matokeo tu ya mwaka huu kuiweka kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Wakali hao wa Etihad walionyakua mataji matatu makubwa kwa msimu wa 2022-23 baada ya kuwasha moto na kuwapiku Arsenal dakika za mwisho kwenye Ligi Kuu England, wameanza msimu huu kwa kasi, wakishinda mechi sita za mwanzo kabla ya kukumbana na vipigo viwili mfululizo kutoka kwa Wolves na Arsenal.

Nafasi inayoshtua zaidi ni ile inayoshika Chelsea. Kwa msimu wa Ligi Kuu England kwa mwaka huu wa 2023, Chelsea inashika namba za chini sana, ikiwa imezizidi Everton na Bournemouth pekee kwenye orodha ya timu zilizovuna pointi nyingi kwenye ligi hiyo tangu mwaka huu ulipoanza.

The Blues ina wastani wa kuvuna pungufu ya pointi moja kwenye mechi zake 27 zilizopita – kiwango ambacho kama itaendelea nacho hadi mwisho wa mwaka huu, basi kama ni ligi basi itashuka daraja.

Kwa kuzingatia msimamo wa Ligi Kuu England, ambao unahusu timu zilizoanza mwaka huu wa 2023, basi Chelsea ipo kwenye orodha ya timu tatu za mkiani.

Msimamo huu hauhusu timu za Burnley, Sheffield United na Luton Town – ambazo zimepanda daraja msimu huu na umeziondoa timu zilizoshuka daraja, Leicester City, Leeds United na Southampton.

Cheki hapo pembeni msimamo wa Ligi Kuu England unavyosoma kwa kuzingatia mechi zilizochezwa ndani ya mwaka huu wa 2023 tangu ulipoanza.

Chanzo: Mwanaspoti