Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea haipoi tu nyie

Josko Gvardiol Rb Leipzig 2022 1646945257 81805 Josko Gvardiol

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Chelsea imeripotiwa ipo kwenye mazungumzo na RB Leipzig kwaajili ya kinda wao Josko Gvardiol, 20, mwenye thamani ya Pauni 77 milioni.

Kocha wa The Blues, Thomas Tuchel tayari amekamilisha usajili wa beki aliyekuwa akikipiga Leicester City, Wesley Fofana.

Lakini nguli wa masuala ya usajili Fabrizio Romano amedai, Tuchel ana matumaini atakamilisha uhamisho wa Gvardiol anayecheza beki wa kati. Aidha endapo beki huyo atakamilisha uhamisho huo atabaki RB Leipzig kukupiga kwa mkopo msimu mzima.

Chelsea wanataka kushinda katika kinyang'anyiro cha Gvardiol huku kukiwa na nia ya dhati kutoka kwa wapinzani wao Man City na Tottenham. Tuchel anataka kupata mkataba wa kitita chaPauni 77 milioni sasa kabla ya kumtoa kwa mkopo Gvardiol kurudi Leipzig kwa msimu huu.

Iwapo Chelsea watapata dili la kumsajili nyota huyo, inaweza kuibua maswali juu ya mustakabali wa Thiago Silva, anatimiza miaka 38, mwezi ujao. Bado kuwasili kwa Gvardiol kunaweza kuashiria kwamba Silva anafikiria kustaafu mwishoni mwa msimu.

Beki huyo kinda atachukuwa mikoba ya Thiago Silva, 38, siku za usoni endapo ataondoka Chelsea kwani umri umemtupa mkono kwasasa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz