Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea gari limewaka, waitandika Nottingham Forest Darajani

IMG 0255.jpeg Chelsea gari limewaka, waitandika Nottingham Forest Darajani

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.

Mabao ya Chelsea yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Ukraine, Mykhailo Mudryk (23) dakika ya nane, washambuliaji Muingereza mwenye asili ya Jamaica, Raheem Shaquille Sterling (29) dakika ya 80 na Msenegal mzaliwa wa Gambia, Nicolas Jackson dakika ya 82.

Kwa upande wao Nottingham Forest mabao yao yamefungwa na beki Muivory Coast, mzaliwa wa Ufaransa, Willy-Arnaud Zobo Boly (33) dakika ya 16 na winga mwenye asili ya Ghana, Callum James Hudson-Odoi (23) dakika ya 74.

Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya saba, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 29 za mechi 37 nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live