Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea bado yatoa macho kusaka mrithi wa Pochettino

De Zerbii (19).jpeg Roberto De Zerbi

Mon, 27 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea haijafuta mpango wa kumpa kazi Roberto De Zerbi kwenda kuchukua mikoba ya Mauricio Pochettino kuinoa miamba hiyo ya Stamford Bridge msimu ujao.

The Blues ipo sokoni kutafuta kocha mpya baada ya Pochettino kuondoka ghafla kwenye timu hiyo aliyoinoa kwa msimu mmoja na kuipa tiketi ya kushiriki kucheza michuano ya Ulaya kwa msimu ujao.

Ripoti zinafichua kwamba miamba hiyo ya London Magharibi imefanya mchakato wa kupunguza makocha inaowafukuzia na kufikia wanne, ambapo mmoja atapewa kazi hiyo katika muda mfupi ujao.

Orodha hiyo inamhusisha pia kocha wa Leicester City, Enzo Maresca, kocha wa Ipswich Town, Kieran McKenna na yule wa Brentford, Thomas Frank.

Bado haijathibitishwa kama ni De Zerbi, 44, ndiye kocha wa nne ambayo hakuwekwa wazi. Na kinachoelezwa ni kwamba Chelsea yenyewe haijafuta mpango wa kumpa kazi Mtaliano huyo baada ya kuachana na Brighton.

Kama Chelsea itamsainidha De Zerbi basi Brighton itakuwa na uhakika wa kupata fidia ya Pauni 5 milioni, kitu ambacho kinatajwa kuwa ni nafuu kuliko ingelipa Pauni 15 milioni kumpata kama angekuwa bado kazini Amex Stadium.

Kocha huyo wa zamani wa Shakhtar Donetsk anaweza kushawishika kwenda kufanya kazi Chelsea, ambapo atakwenda kuungana na wakurugenzi wa michezo, Paul Winstanley na Laurence Stewart.

Hadi sasa hakuna kocha anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Pochettino.

Hata hivyo, Maresca, McKenna na Frank wote wanapata sapoti ya kutoka ndani ya Chelsea.

Chanzo: Mwanaspoti