Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea bado majanga, majeruhi waongezeka

Skysports Football Champions League 5952559 Chilwell akisaidiwa na Madaktari kutoka nje ywa Uwanja

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Chelsea imepata pigo jingine hapo jana baada ya beki wao mwingine Ben Chilwell kuumia kwenye mchezo wa klabu bingwa Ulaya walipokuwa wakicheza dhidi ya Dinamo Zagreb.

Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kushinda kwa mabao 2-1, huku kocha wa timu hiyo Graham Potter akihofia kuwa huenda mchezaji huyo asipone kwa haraka baada ya kutoka uwanjani akichechemea, huku zikiwa zimesalia siku 19 tu kabla ya England kuanza kampeni yao ya kombe la Dunia.

Kwahiyo mpaka sasa Potter ana wachezaji wawili ambao ni majeruhi katika eneo hilo la beki wa pembeni wa kwanza akiwa ni Recce James aliyeumia kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Milan na sasa Ben Chilwell nae ameumia.

Chelsea walitanguliwa kufungwa bao mapema kabisa katika dakika ya 7 ya mchezo na baadae Sterling akaja kusawazisha bao hilo, lakini ndani ya dakika 45 za kwanza The Blues walipata bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Denis Zakaria huku ikiwa ndiyo mechi yake ya kwanza kucheza toka atue Darajani.

Potter amekiri kuwa jeraha la beki huyo wa kushoto linaonekana “sio kubwa” na kuwaacha Chelsea na England wakiwa na wasiwasi juu ya utimamu wa beki huyo wa kushoto huku akisema kuwa hana matumaini kwa sasa kuhusu jeraha la Chilwell na ni pigo kwao baada ya mchezo mzuri .

Potter amekuwa kocha wa kwanza wa Chelsea tangu Roberto Di Matteo, ambaye alishinda Kombe hilo msimu wa 2011-12, kutopoteza katika mechi zake tano za kwanza za Ligi ya Mabingwa akiwa kocha.

The Blues tayari walikuwa wamefuzu kwa hatua ya mtoano wakiwa vinara wa Kundi E, baada ya kushinda mechi zao nne, sare moja na kipigo mara moja, huku Graham akiiambia BT Sport kuwa;

“Nimefurahishwa sana kupata ushindi huo. Nilidhani Denis alikuwa mzuri sana, alicheza kwa ari alisonga mbele na nimefurahishwa naye. Ilikuwa mechi nzuri ya kwanza. Wasiwasi utakuwa kama hautengenezi nafasi, lakini nia yetu ilikuwa nzuri, uchezaji wetu ulikuwa mzuri na ubora ulikuwepo kutoka kwa wachezaji”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live