Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea, Olise mpango upo hivi

Oliseeeee Chelsea, Olise mpango upo hivi

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea imefikia makubaliano na winga wa Crystal Palace Michael Olise, 22, kwa ajili ya kumsajili dirisha hili na sasa inafanya mazungumzo na mabosi wa Palace kwa ajili ya kufikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho.

Olise ambaye amewahi kuhusishwa na Liverpool inayomwangalia kama mbadala wa Mohamed Salah ambaye huenda akaondoka mwisho wa msimu huu.

Mbali ya Liverpool, tajiri wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe pia ameweka kipaumbele cha kumsajili staa huyu katika dirisha hili.

Licha ya makubaliano binafsi ambayo Chelsea imefanya na staa huyu, kuna uwezekano pia dili likafeli kwenye nyanja ya ada ya uhamisho kwani mkataba wa Olise unaeleza Palace inatakiwa kujadiliana naye ada ya uhamisho ambayo haitopungua Pauni 35 milioni, kisha mchezaji mwenyewe ndio awasiliane na Chelsea kuwaambia anauzwa kwa kiasi fulani.

Awali ilielezwa, mkataba wake una kipengele cha kumsajili kwa Pauni 35 milioni, lakini baada ya kusaini dili jipya la miaka minne kipengele hicho kimekufa na sasa Palace itahitaji walau Pauni 60 milioni ili kumuuza.

Kiasi hicho cha pesa kinaonekana kuwa ni kikubwa sana kwa Chelsea ambayo inataka kubana matumizi katika dirisha hili ili isije kupigwa rungu na mamlaka za soka England kwa kukiuka kanuni za matumizi ya pesa.

Chanzo: Mwanaspoti