Huenda akawa ndie Straika anaewindwa zaidi barani Ulaya kwa sasa kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu.
Kuna vilabu kadhaa vinavyoonyesha nia ya kuhitaji saini ya kinda huyo ambae anaimarika kila kunapokucha.
Sasa Chelsea na Manchester United, miongoni mwa vilabu vinavyoonesha nia ya kumtaka Haaland, zimepewa onyo kuwa Straika huyo hatauzwa kwa bei chee kama wanavodhani.
Kwa mujibu wa ripoti, Haaland ataigharimu Chelsea na Man United kitita cha Pauni 250 milioni, hiyo kwa mujibu wa wakala wake Mino Raiola.
Dormund haipo tayari kumwachia kirahisi fowadi wao huyo, endapo ofa nzuri itatolewa huku Man United na Chelsea zikipigana vikumbo kuwania saini yake.
Haaland ameonyesha kiwango bora tangu alipotua Dortmund akiwa amefunga jumla ya mabao 70 katika mechi alizocheza mashindano yote.
Kwa sasa yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha aliyoyapata mwezi uliopita, na kutoonekana kwake imekuwa pigo kubwa kwa Dortmund.