Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea, Man City zapigana vikumbo kwa Bastoni

Alessandro Bastoni Alessandro Bastoni.

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu za Chelsea na Manchester City zote zinafuatilia uhamisho wa beki wa Inter Milan na Timu ya Taifa ya Italia, Alessandro Bastoni.

Baada ya kuanza soka kama beki wa pembeni, Bastoni amebadilika na kuwa beki wa kati ambaye amekuwa muhimu kwa klabu na nchi yake.

Muitaliano huyo aling’ara wakati Inter ilipotinga fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora wa kati barani Ulaya kwa sasa.

Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino ana safu ya mabeki wa kati wakiwemo mabeki wapya Axel Disasi, Benoit Badiashile na Wesley Fofana, huku Levi Colwill akiwa chaguo jingine nafasi hiyo.

Hata hivyo, Silva anasalia kuwa kinara wa ulinzi na kuondoka kwake mwisho wa msimu huu kutahitaji mbadala wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live