Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea, Arsenal jino kwa jino kwa Williams

Nico Williams Nico Williams

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea bado ina mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Nico Williams ambaye anawindwa na Arsenal ambayo inadaiwa kumpa ofa kubwa itakayoenda kumfanya kuwa mchezaji namba mbili kwa kulipwa zaidi katika kikosi cha washika mitutu hao.

Williams ambaye amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Hispania kwenye michuano ya Euro inayoendelea huko Ujerumani, mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa staa huyu na aliwaambia mabosi wake kwamba wafanya kila linalowezekana ili kiungo huyo atue.

Bilbao ipo tayari kumwachia ikiwa timu inayomhitaji itatoa ada ya kuvunja mkataba wake inayodaiwa kuwa ni Euro 55 milioni ambayo inaweza kulipwa na timu hizi mbili.

Katika msimu uliopita, alicheza mechi 39 za michuano yote, akafunga mabao nane na kutoa asisti 19.

Chanzo: Mwanaspoti