Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chelsea, Arsenal hakuna Mbabe

IMG 6057.jpeg Mchezo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa London, Timu ya Chelsea wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumamosi Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

Chelsea ilitangulia kwa mabao ya Cole Palmer dakika ya 15 kwa penalti na Mykhailo Mudryk dakika ya 48, kabla ya Arsenal kuzinduka na mabao ya Declan Rice dakika ya 77 na Leandro Trossard dakika ya 84.

Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Arsenal inafikisha pointi 21 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao ya Mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live