Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cheki namba za Yanga zilivyoitesa Simba

Yanga Simba Nov 20.jpeg Cheki namba za Yanga zilivyoitesa Simba

Wed, 15 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Achana na Simba kukosa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2021/22, 2022/23 na msimu huu, lakini wana Msimbazi wamepitia nyakati ngumu zaidi kuanzia pointi hadi mabao ya kufunga mbele ya mabingwa, Yanga huku namba na ufanisi uwanjani pia vikiwa mtihani kwa Simba.

Yanga imetwaa taji la 30 na la tatu mfululizo msimu huu ikiandika rekodi nyingi kuanzia kufunga mabao mengi, kukusanya pointi nyingi na kuzifunga timu zote 15 inazocheza nazo mashindano hayo, lakini kwa upande wa Simba mambo ni magumu.

Mbali na Yanga kuipita Simba kwenye kutwaa taji msimu huu, pia imewapita wapinzani wao kwenye maeneo haya.

KUONGOZA LIGI

Yanga imetwaa taji ikimtesa Simba kwenye nafasi ya kuongoza msimamo, Simba msimu huu imekaa kileleni mwa msimamo mzunguko wa tano tangu hapo vita ikawa kati ya mabingwa na Azam FC.

Misimu miwili nyuma ambayo Yanga ilitwaa ubingwa Simba ndio timu ambayo ilikuwa inakamata nafasi ya pili tofauti na msimu huu ambao inalega lega na kuingia vitani na Azam FC kuwania nafasi hiyo.

POINTI 10 NYUMA YA YANGA

Yanga imetetea taji la msimu huu ikiwa bado ina michezo mitatu mkononi hii ni baada ya kuwafunika wapinzani wake Simba na Yanga kwenye ukusanyaji wa pointi kwenye mechio walizocheza.

Yanga msimu huu imechukua pointi kwa timu zote 15 hivyo imefanikiwa kukusanya pointi nyingi kwenye mechi 26 wamekusanya pointi 68 huku watani wao Simba wao kwenye michezo 26 wana pointi 57 wakiachwa nyuma kwa pointi 10.

KURUHUSU MABAO

Wakati Yanga ikitangazwa kuwa mabingwa wa msimu huu tayari ilikuwa imeruhusu mabao 13 huku Simba nyavu zao zikitikiswa mara 24 kati ya mechi 26 walizocheza.

Ukuta wa Simba unaundwa na mabeki wa kati wa kigeni Henock Inonga na Che Malone Fondoh, huku upande wa Yanga imeruhusu idadi ndogo ya mabao ukuta wao ukiundwa na wazawa Ibrahim Hamad 'Bacca', Bakari Mwamnyeto wakisaidiana na Dickson Job.

KUTOA POINTI SITA KWA WATANI

Baada ya miaka mingi kupita msimu huu Yanga ikiwa bora imefanikiwa kukusanya pointi sita kutoka kwa watani wao Simba baada ya kuwafunga nje ndani.

Simba mbali na kutoa pointi zote sita dhidi ya Yanga imeweka rekodi ya kufungwa mabao saba ndani ya msimu mmoja wakikubali kichapo cha mabao 5-1 nyumbani na mzunguko wa pili walifungwa mabao 2-1.

SAFU YA USHAMBULIAJI

Msimu huu mabingwa ndio vinara wa upachikaji wa mabao wakiongozwa na kiungo wao mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye amehusika kwenye mabao 23 kati ya 60 yaliyofungwa na timu yake akiingia kambani mara 15 na kutoa pasi za mwisho nane.

Yanga ambayo viungo ndio wanaongoza kupachika mabao imefunga mabao 60 kwenye michezo 26 waliyocheza huku watani zao Simba wao wakifunga mabao 51 wameachwa nyuma mabao tisa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: