Beki mkongwe wa kimataifa wa Kenya David Ochieng “Cheche” amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Mathare United dili litakalomfanya mchezaji huyo kubakia klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu huu.
Mathare United ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL inamrejesha Cheche ikiwa ni awamu ya pili baada ya kitasa huyo kuitumikia klabu hiyo msimu wa mwaka 2020/21.
Ujio wa mlinzi huyo ni kusaidia na wachezaji wengine kuhakikisha klabu hiyo inabakia kunako Ligi Kuu ya KPL kwani alikuwa hana timu baada ya kuachana na Posta Rangers.
Dirisha dogo la usajili nchini Kenya linafunguliwa rasmi Jumatatu ya Februari 27 ambapo hata mchezaji huyo ndiyo siku ambayo atakuwa halali kutumika.