Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Che Malone ajivunia kuingia fainali ya kwanza Simba

 Che Fondoh Malone.jpeg Che Malone ajivunia kuingia fainali ya kwanza Simba

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kisiki wa Simba SC, Che Malone, amesema anajivuninia kushiriki mashindano ya kwanza ya Simba na kuingia fainali.

Che Malone amayasema hayo jana Januari 10, 2024 mara baada ya kufanikiwa kuitoa Singida FG katika mchezo wa nusu Fainali ya Mapinduzi Cup yanayoendelea visiwani Zanzibar.

"Najivunia ni mashindano yangu ya kwanza nikiwa na Simba na nimeingia fainali, natamani sana kuicheza hiyo fainali na ninaamini tunakwenda kupata ushindi na kuchukua kombe," alisema Che Malone.

Che Malone ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na Simba baada ya kusajiliwa katika dirisha kubwa la usajili kwa msimu wa 2023-24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live