Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chasambi: Msimu ujao Simba tutafanya balaa

Ladack Chasambi Simba Ladaki Chasambi

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji, Ladaki Chasambi amesema ana matumaini msimu ujao watafanya vizuri kutokana na maandalizi na kikosi tulichonacho.

Chasambi amesema kikosi chao kimeundwa na wachezaji wengi vijana na wapo tayari kuipambania timu kuhakikisha tunafanya vizuri.

Chasambi ameongeza kuwa maandalizi wanayofanya kupitia benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids ni mazuri na hayo yanampa matumaini kuwa msimu ujao tutakuwa bora zaidi.

“Kambi yetu ni nzuri hapa Misri, tunafanya mazoezi chini ya Kocha Fadlu na wasaidizi wake na kila kitu kinaenda sawa na tunaamini tutakuwa bora zaidi msimu ujao.”

“Timu yetu inaundwa na wachezaji vijana na tuna ari ya kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuirejesha Simba katika nafasi yake iliyokuwepo,” amesema Chasambi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live