Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanzo cha utani wa jadi Simba na Yanga

Yanga Azam Mudathiri Chanzo cha utani wa jadi Simba na Yanga

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Juzi pale ilipigwa gemu la watani wa jadi, Simba na Yanga. Ni mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii na taji hilo likienda Msimbazi.

Yanga ilitinga fainali baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 huku Simba ikishinda kwa penalti 4-2 dhidi ya Singida Fountain Gate baada ya sare tasa.

UTANI WA JADI

Kwetu hapa Dar es Salaam na mikoa mingine, watani huzikana. Watu wa kabila fulani wakipatwa na msiba au janga lolote watu wa kabila lingine ambao ni watani hufika kutoa huduma. Wakati huduma hii ikitolewa, wafiwa husimangwa na kutukanwa.

Hili ni jambo la ajabu sana kwa watu wasiouzoea utamaduni huu lakini ni la kawaida kwa makabila husika.

Huduma hutolewa lakini huja kwa masimango na matusi. Huu ni utani wa kuzikana.

SABABU YA UTANI

Utani huja kwa sababu maalumu, mara nyingi makabila yenye utani yalikuwa na uhusiano fulani huko nyuma, huenda walipigana vita vya jadi au labda babu zao walikuwa pamoja kisha wakafarakana.

Wakati mwingine lugha za watani hufanana, katika hali kama hii kabila fulani huwacheka wenzao kwasababu wanabadilisha namna ya kuzungumza baadhi ya maneno.

UTANI WA SIMBA NA YANGA

Masikani ya klabu hizi ni Kariakoo jijini Dar es Salaam, enzi hizo mji huu ukiwa na zaidi ya watu laki tano (500,000) kwa hesabu za mwaka 1975, kulikuwa na klabu 15 tu vya mpira wa miguu.

Ni klabu tatu tu ndizo zilizokuwa maarufu, kwanza watani wa jadi, Simba na Yanga kisha Cosmopolitans au Cosmo ambayo ilisimama katikati ya utani wa jadi, kuna wakati iliiadhibu Yanga na kuna wakati iliidhabu Simba wakati mwingine na yenyewe iliadhibiwa na timu hizo.

Ilikuwa furaha kwa mashabiki wa Simba kuiona Comso ikiifunga Yanga. Pia mashabiki wa Yanga walifurahi Cosmo ilipoiadhibu Simba.

KWANINI WATANI WA JADI?

Imekuwaje hadi Simba na Yanga zimekuwa watani wa jadi? Zamani zilikuwa ni kitu kimoja. Umoja wa Waafrika (Watanganyika) ulishikana sana enzi hizo dhidi ya mkoloni, Muingereza alipotawala baada ya vita kuu ya kwanza. Muingereza alileta michezo ya gofu, tenisi, kriketi na kandanda. Michezo hii ilikuwa ni kati ya Wazungu na vibaraka wao, Wahindi. Waafrika walikuwa wakikodolea macho.

WAAFRIKA WAKUSANYIKA

Mwaka 1926, vijana wa kizalendo walikusanyika katika mti mmoja pale Jangwani, Dar es Salaam na kuanzisha wazo lao la kucheza chandimu kama mpira wa kienyeji unavyojulikana. Waliita timu yao Jangwani. Timu haikuwa na mpira rasmi, viatu, jezi wala bukta.

Timu ilisokota matambaa na kutengeneza mfano wa mpira na kucheza bila ya kuwa na vifaa vingine.

WATU WA MAARUFU

Siku za mwanzo Jangwani haikufahamika siku za mwanzo kwani haikufika hata daraja la pili, watu maarufu kipindi hicho walikuwa ni kina Kondo Kipwata na Mangara Tabu Mangara (waliwakuwa kuwa wenyeviti wa Yanga), Masoud Mwinchande, Ramadhan Maulid Kasongo, Abdul Hija.

Wanachama wengi wa timu hiyo walikuwa wakifanya kazi bandarini ndio maama hata wachezaji wengi wa Simba na Yanga baadaye walipata kazi bandarini.

Kufanya kazi bandarini kuliwafanya wawe na nafasi ya kufahamiana na kuzungumzia soka na waliwashawishi wengine kujiunga na Jangwani.

Kutokana na kufanya kazi bandarini kuliifanya timu hiyo kubadili jina na kujiita Navigation na haukupita muda mrefu ikapata umaaarufu mkubwa.

Jangwani ilifanikiwa kuzinyanyasa timu za Gerezani, Mtendeni, Kisutu na Kitumbini baadaye timu ikabadili jina na kujiita Taliana kujifananisha na uzungu wa Italia ambao walikuwa wakisifika kwa kusakataka kabumbu.

SASA IKAWA YOUNG BOYS

Ujasiri wa uongozi wa timu ya Taliana ukaifanya timu isonge hadi Ligi Daraja la Pili na kuwafanya vijana wazalendo na kuuita New Young Boys yaani vijana wapya.

New Young Boys ilitamba sana na kufanikiwa kubeba kombe la Kassum baada ya kuzifunga timu kadhaa za Dar es Salaam.

Hadi mwaka 1937 timu hii ilikuwa kali sana na hata wazungu wakaanza kuiogopa ingawaje haikuwa na viatu vya kuchezea mpira.

Chanzo: Mwanaspoti