Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Championship balaa lake sio mchezo

Katwila Pic Data Zuber Katwila wa kwanza kushoto

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha wa Ihefu FC, Zuber Katwila amekiri kuwa Ligi ya Championship ina ushindani mkubwa kuliko Ligi Kuu Bara.

Katwila kocha aliyetua Ihefu msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar ili kuwaokoa wasishuke daraja lakini jitihada zake ziligonga mwamba kwani timu hiyo ilishuka daraja ikiwa imeshiriki Ligi Kuu msimu mmoja pekee.

Akizungumza na gazeti hili, Katwila amesema kuwa ushindani wao sasa ni mkubwa na hasa ikizingatiwa kila timu inapambana kupanda Ligi Kuu hivyo kila mchezo wanaokutana nao unakuwa kama fainali.

“Kila mara nazungumza na wachezaji wangu nawataka wapambane kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika kila mchezo ili kuwa na uhakika mapema.

“Tukiwa na matokeo mazuri hata huko mbele hatutakuwa na presha hata kidogo maana tunakuwa tumepata uhakika kabisa wa kupanda daraja, lakini ushindani ni mkubwa na ligi ni ngumu,” amesema Katwila

Amesema malengo yake ni kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Bara ambayo pia ina ushindani wa vita ya kubaki na kushuka

DTB inayoundwa na mastaa kibao walicheza Ligi Kuu Tanzania Bara siku za nyuma ndiyo vinara wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.

Timu mbili zitapanda Ligi Kuu moja kwa moja.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz