Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chambua amchambua Kagere

80686 Pic+chambua

Fri, 18 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

STRAIKA wa Simba Meddie Kagere anaendelea kujitengenezea ufalme wake kwenye Ligi Kuu Bara, kama alivyosema mchezaji wa zamani wa Yanga, , Sekilojo Chambua kwamba anamuona kuwa ndiye straika hatari zaidi kwa sasa.

Chambua amesema washambuliaji wazawa wanapaswa kuiga mfano wa Kagere ambaye muda wote akili yake ipo kuzifuma nyavu kwamba ndivyo inavyotakiwa Simba na Yanga kuwa na mchezaji wa aina hiyo.

Amemchambua Kagere kwamba ametambua nafasi yake na mahitaji ya Simba kwamba inataka nini kwake, jambo analoamini linampa juhudi ya kufanya vizuri zaidi.

"Mchezaji mzuri ni yule ambaye analinda kiwango chake, Kagere ndiye alikuwa mfungaji bora msimu ulioisha na sasa anaonekana anatamani kufanya kitu kikubwa zaidi,"

"Awe somo kwa washambuliaji wote wa ligi kuu, kujua nafasi zao na iwe inawauma pindi inapotokea hawajafunga, Kagere anafunga kila mechi hii inaonyesha kwamba ni mshambuliaji wa kweli na hababaishi,"amesema.

Huu ni msimu wa pili kwa Kagere kucheza Ligi Kuu Bara, Simba ilipomsajili kutoka Gor Mahia ya Kenya, msimu ulioisha alikuwa mfungaji bora akifunga mabao 23 na sasa anaongoza kwa mabao sita.

Chanzo: mwananchi.co.tz