Mchambuzi wa soka nchini Tanzania Ibrahim Maestro ameamua kutoa ya Moyoni dhidi ya sakata la mchezaji wa Kimataifa wa Simba SC Raia wa Zambia Cloutos Chama kuhusu swala la mchezaji huyo kuomba kuondoka Simba au kuboreshewa maslahi yake.
Akizungumza katika kipindi cha michezo cha EFM asubuhi ya jana Maestro amesema; “Kama Chama anafanya hizi drama kila msimu tuseme nini? Anatafuta followers au anataka ku'Trend? kila new season ana make headline”
Chama amesema mwenyewe kuwa kuna timu imekuja mezani kumtaka alipoulizwa ni timu gani akasema ni siri , Chama awatazame mashabiki wanaomshangilia, siyo kila siku yeye tu" amesema Maestro
Kiungo huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Simba SC ila amewataka viongozi wa Simba kuuboresha (maslahi yaongezwe) akisema ni makubaliano yaliyokuwepo kati yake na mtendaji mkuu aliyeondoka Barbara Gonzalez yakukaa kila msimu unapomalizika kuongeza maslahi yake
Viongozi wa Simba wamekamilisha jukumu lao lakumalizia sehemu ya pesa aliyokua anadai mchezaji huyo ambapo amechiwa jukumu la kuamua hatma yake ikiwemo, kupeleka ofa aliyoipata mezani ofa ambayo kwa mujibu wake ni siri yake au aungane na wachezaji wenzake kambini Uturuki kwa maandalizi ya msimu mpya, huku wakiweza wazi hawatakuwa tayari kwa maboresho yoyote ya kimkataba kwa kuwa hakuna kipengele kwenye mkataba wake kinachosema hivyo!