Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama ni mvivu - Mchambuzi

Simba Vs Namungo Chama Chama ni mvivu - Mchambuzi

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Saviour John amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' ni mvivu kwani hupenda kucheza taratibu jambo ambalo linasababisha makocha wengi wanaokuja Simba Sc wamekuwa wakimkataa.

Saviour John amesema hayo mara baada ya ujio wa Kocha mpya, Abdelhak Benchikha kuanza kumpiga benchi Chama katika mechi mbili za mwanzo.

Ikumbukwe kuwa, wakati anakuja Simba kocha Robertinho wakati wa dirisha dogo msimu uliopita, alikuwa akimfanyia mabadiliko Chama kipindi cha kwanza tu cha mchezo jambo lililosababisha mashabiki wa timu hiyo kupiga kelele.

"Chama ni mvivu lakini ni mbunifu, anapenda kukaa na mpira ila Kibu Denis, Onana ni watu wanaokimbia timu inaweza ikawa mbele ila mpira akawa nao Chama ana-dribble taratibu.

"Kocha Benchika anachokihitaji ni ukiwa na mpira kimbia, uwe na mawazo ya haraka ufanye maamuzi sahihi na ndio sababu ya Chama kuanzia benchi," amesema Saviour John.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live