Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama na Inonga ni tatizo pale Simba, waondolewe

Realclatouschama Clatous Chama.

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Wasafi FM, Nasri Khalfani amedai kuwa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Clatous Chama amekuwa sehemu ya matatizo ya klabu hiyo.

Nasri amesema kuwa viongozi Simba wanatakiwa kutowaonea huruma na kuwaondoa wachezaji wanaojiona wao ni wakubwa kuliko klabu kwani ndiyo wanaosababisha timu ishindwe kufanya vizuri akiwemo Chama na henock Inonga.

“Chama ni miongoni mwa matatizo ya Simba lakini viongozi wa Simba hawajaweza kulishughulikia hilo tatizo. Mwanzoni mwa msimu huu ni Chama huyu huyu aligoma kusafiri na timu kwenda pre-season Uturuki kwa ajili ya maandilizi kuelekea msimu mpya.

“Wakati timu inajiandaa na msimu mpya unategemea mchezaji muhimu kama Chama awepo kwenye hayo maandalizi ili ajue atatumikaje msimu ujao na mchango wake utakuwaje msimu unaofuata, akagoma kusafiri na kundi la wachezaji wenzake.

“Mkataba alikuwa bado anao, na mchezaji ana uongozi wake kwa hiyo jukumu lake ni kutimiza majukumu ndani ya uwanja kisha masuala yake ya kimkataba na klabu anauachia uongozi wake unashughulikia. Kama asingekuwa na mkataba alikuwa sahihi kubaki lakini yeye mkataba wake alikuwa na mkataba wa mwaka mzima, kwa hiyo Chama alikuwa miongoni mwa matatizo ya Simba.

“Chama ameanza msimu vizuri, hapa katikati akafanya mambo aliyofanya akasimamishwa, amekuja kurejea kwenye kikosi siku zimekwenda na timu inataka kupambana ipate ubingwa wakati mchezaji wake muhimu kama Chama hayupo. Maana yake ameiathiri klabu kwa uzembe wake binafsi.

“Simba wangepima tu kwamba huyu mchezaji vipi na kwa hali ilipofikia, mkataba umeisha, umri kidogo umeenda na ni mchezaji msumbufu kwa klabu, ni bora wakaachana naye kuangalia wanaendaje mbele bila Chama. Huyu Chama alikuwepo msimu uliopita, aliisaidia nini Simba? Alifanikisha malengo gani? Hakuna malengo yoyote walifanikisha na Chama alikuwepo, bora wakaachana naye.

“Inonga aliona kwa Chama kwamba hii klabu ukiisusia haina ya kukufanya, watakubembeleza kisha wakurudishe kikosini. Hapa mwishoni Inonga alijivunja kumbe hakuumia chochote, akaonekana yuko Paris Ufaransa anakula kuku.

“Hivi vitu vinavyoendelea Simba huwezi kuviona Yanga, klabu ambayo iko serious. Yanga walianza kuliona hilo kwa baadhi ya wachezaji msimu uliopita, msimu ulipomalizika tu wakawaondoa kikosini. Simba wachezaji ambao hawana mioyo ya kuitumikia klabu wanawabakisha na wanaharibia hata wachezaji wazuri, kwa hiyo hiki kinachoendelea Simba si kwa bahati mbaya, Inonga alishaona kwa Chama anafanya vitu kama hivyo,” amesema Nasri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live