Kiungo hatari wa Simba Clatous Chotta Chama,anatajwa kutakiwa na moja ya Klabu kubwa nchini Morocco.
Kiungo huyo ambae ni kipenzi cha mashabiki wa Msimbazi anatajwa kuondoka ikiwa ni siku chache tu tangu kuondoka kwa nyota mwingine wa Klabu hiyo, Luis Miquissone aliyetimkia klabu ya Al-ahly ya nchini Misri.
Vyanzo vya Uhakika kutoka ndani ya klabu ya simba, vimesema hata Mtendaji mkuu wa Simba Babra yupo nchini Morocco japo haijawekwa wazi sana sababu za kuwepo huko aidha kukamilisha dili hilo ama kwa kuwa klabu ya simba pia inakwenda kuweka kambi nchini Morocco.
Chama raia wa Zambia,amefika robo fainali mbili za klabu bingwa Barani Afrika akiwa na klabu ya Simba. Chama tayari amewasili nchini kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.