Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama la Masau lazitaka tatu Polisi

Ruvu Pic Chama la Masau lazitaka tatu Polisi

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wazee wa Kupapasa, Ruvu Shooting imeendelea kujifua kwa maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania ilitopangwa kupigwa Aprili Mosi huku kocha Mkuu wa wajeshi hao Boniface Mkwasa akikomaa na alama tatu za mechi hiyo.

Mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi itakuwa ya kisasi kwa Ruvu Shooting ya Mkwasa kwani kwenye mzunguko wa kwanza ilipoteza nyumbani kwa kuchapwa bao 1-0 na maafande hao wa Polisi lakini pia itakuwa ikipigania alama tatu zitakazoipandisha nafasi tano.

Kocha Mkwasa amefunguka kuwa kutokana na mwenendo wa ligi ilivyo msimu huu, wanahitaji kushinda mechi hiyo ili kutengeneza mazingira ya kubaki ligi kuu msimu ujao.

“Hii ni mechi muhimu sana kwetu. tunahitaji kushinda ili kutoka huku chini tuliko, tunaijua Polisi ni timu imara lakini tunahitaji zaidi ushindi hivyo mazoezi na programu zote za mazoezi tumefanya kwa kipaumbele cha kwenda kutafuta ushindi tu,” alisema Mkwasa na kuongeza;

“Viongozi, wachezaji na benchi la ufundi wote nimewaeleza umuhimu wa alama tatu kwenye mechi hiyo hivyo tunachosubiri ni muda ufike tukapambanie kile tunavhokitaka.”

Naye Winga wa timu hiyo, Pius Buswita kwa niaba ya wachezaji ameeleza kuwa tayari kupambana na kuhakikisha wanashinda mechi hiyo na kupata matokeo chanya kwenye mechi zilizobaki.

“Tunahitaji kufanya vizuri ili kupunguza presha kikosini. Kama wachezaji tupo tayari kufanya hivyo na tunaamini tutafanikiwa kwani morali ya kila mmoja wetu iko ju,” alisema nyota huyo wa zamani wa Mbao, Yanga na Polisi Tanzania.

Ruvu ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 20 na endapo ikishinda dhidi ya Polisi yenye alama 22, itafikisha pointi 23 na kupanda hadi nafasi ya saba ambayo itakuwa salama kwao kuelekea mwisho wa msimu na itakuwa imebakiza mechi 11 tu kumaliza ligi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz