Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama kuondoka nchini Ijumaa

Chama Complete Chama kuondoka nchini Ijumaa

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaje wa Simba SC, anatarajia kuondoka nchini Ijumaa Julai 21, 2023 kuelekea nchini Uturuki kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu 2023-24.

Awali kulikuwa na sintofahamu juu ya Chama kama atasalia Msimbazi au la baada ya wenzake kusafiri na yeye kubaki Dar huku kukiwa na tetesi kuwa anahitaji kuongezewa mshahara ikiwa ni sehemu ya mkataba wake na klabu.

Hata hivyo, leo Julai 17, 2023, majira ya saa 9 Alasiri, Simba walitangaza kumalizana na Chama.

"Tabu ipo pale pale kwa wapinzani, Clatous Chama na Fabrice Ngoma siku ya Ijumaa Julai 21, 2023 wataanza safari kwenda kwenye kambi yetu nchini Uturuki. #NguvuMoja," waliandika Simba Twitter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live