Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama hapoi, atua na kuanza tizi fasta!

Chama Hapoi, Atua Na Kuanza Tizi Fasta! Chama hapoi, atua na kuanza tizi fasta!

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama, jana asubuhi amefika nchini akitokea nchini kwao Zambia katika majukumu ya timu ya Taifa na fasta akaelekea Bunju kujumuika na wenzake kwenye mazoezi.

Chama ambaye ni kiungo muhimu na mhimili wa timu, alikuwa sehemu ya Timu ya Taifa ya Zambia iliyoshinda goli 3-0 dhidi ya Uganda mechi ya kirafiki na kurejea kwake salama, kunashusha presha ya mashabiki ambao walikuwa na wasiwasi kwa kutomuona mazoezini.

Nyota mwingine wa Simba muhimu ambaye aliingia jana usiku ni Henock Inonga ambaye naye alikuwa kwenye majukumu ya Timu ya Taifa ya Congo na leo anatarajia kuanza mazoezi na wenzake hii leo.

Simba SC kesho wanatarajia kushuka dimbani katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la African Football Legue, kombe la kwanza kuanzishwa Afrika hivyo kuwa mechi ya kihistoria na ufunguzi wa mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live