Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama hakamatiki kwa assist, aongeza idadi dhidi ya KMC

Chama Sakho Chama hakamatiki kwa assist, aongeza idadi dhidi ya KMC

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam Mwamba wa Lusaka Cleotus Chota Chama 'Triple C' jana amefikisha Asist ya 10 wakati timu yake ikipeleka zawadi ya Kristimas kwa kuibuka na ushindi wa bao 3- 1 dhidi ya timu ya KMC yenye maskani yake Kinondoni.

Kabla ya mchezo wa leo kati ya Simba na KMC uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Chama alikuwa anazo kibindoni Asist 9 na kupitia mchezo huo amefikisha Asist( pasi inayozaa bao) na hivyoinamfanya kuwa kinara wa Asist kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Wakati Chama anaongoza kwa kutoa Asist mshambuliaji hatari wa Klabu ya Yanga Fiston Kalala Mayele yeye ameendelea kuwa kinara wa ufungaji kwa kuwa hadi sasa amefikisha mabao 14 huku mshambuliaji wa Simba Mosses Phiri akimfuatia kwa na mabao 10.

Katika mchezo wa leo kati ya Simba na KMC Chama alitoa Asisti iliyotokana na mpira wa kona aliyopiga iliyomfikia beki kitasa wa timu yake Enock Inonga Banka aliyefunga kwa kupiga kichwa kilichokwenda moja kwa moja langoni mwa KMC.

Chama ambaye amekuwa kwenye ubora kubwa wa kusakata kabumbu alionekana kuisumbua ngome ya KMC.Simba walipata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake John Raphael Bocco baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.

Katika mchezo huo uliokuwa na kasi kwa kila timu kujaribu kwenda kwenye lango la mpinzani wake KMC walifanikiwa kusawazisha bao hilo na hivyo kuwa 1-1.

Hata hivyo baada ya KMC kusawawisha Simba wakionekana wakiongeza kasi ya kushambulia na kuiweka KMC katika kuzuia mashambulizi.

Kasi ya mashambulizi ya Simba yalionekana kuwaweka kwenye wakati mgumu KMC ,hivyo Simba wakapata bao la pili kupitia mchezaji wake Agastine Okra baada ya piga nikupige.

Kwa matoke ambayo Simba wameyapata wanafikisha alama 41 na hivyo kuzidiwa na vinara wa ligi hiyo Yanga ambao wamefikisha alama 47.Hivyo Simba ikiwa nyuma kwa alama Sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live