Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama chini ya uangalizi maalum Simba SC

Chama Na Matola Selemani Matola na Chama

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kiungo wa Simba, Clatous Chama amerejea nchini na juzi asubuhi alitinga mazoezini pamoja na nyota waliokuwa timu za taifa akiwamo Rally Bwalya na fasta Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola akampa programu maalumu ili awe kwenye ubora wake.

Chama aliyekuwa Zambia kwa matatizo binafsi, alikuwa sehemu ya wachezaji wa Simba waliopiga tizi jana asubuhi kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena chini ya Matola na Eliutery ‘Kanka’ Terry.

Akizungumza na Matola, alisema Chama bado hajawa fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha yaliyomweka nje ya uwanja muda mrefu na kusababisha kushuka kiwango chake.

“Nimempa mazoezi peke yake kabla ya kuungana na wenzake moja kwa moja, lengo ni kumrejesha kwenye utimamu, hivyo mashabiki wasiwe na hofu juu yake kwani jambo kubwa ni kuendelea kuisapoti timu,” alisema Matola

Kocha huyo alisema hakuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi kitakachoanza michezo mbalimbali tofauti na mtangulizi wake, Pablo Franco kwani anachozingatia ni kumpa nafasi mchezaji kutokana na kujituma kwake mazoezini.

Meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyimamu alisema wachezaji kama Meddie Kagere, Chris Mugalu, Peter Banda na Shomari Kapombe watarejea muda wowote.

Waliofanya mazoezi jana kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena ni, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Ahmed Feruzi, Pascal Wawa, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Gadiel Michael, Israel Mwenda, Kennedy Juma, Joash Onyango na Henock Inonga.

Wengine ni Chama, Rally Bwalya, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Mzamiru Yassin, Taddeo Lwanga, Pape Sakho, Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, Yusuph Mhilu na John Bocco.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz