Bado kuna sintofahamu juu ya mustakabli wa kiungo Clatous Chama ndani ya Simba SC baada ya kundi la pili la wachezaji kuondoka kuelekea Uturuki kuungana na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya (pre-season) huku Mzambia huyo akiendelea kusalia Nchini.
Akizungumzia suala la Mwamba wa Lusaka, Meneja wa habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ameripotiwa kubainisha kuwa suala na Chama linashughulikiwa na uongozi wa juu.
“Kundi la pili limeondoka alfajiri ya leo na Chama hajaondoka kwenda Uturuki, suala lake lipo katika uongozi wa juu wakijaribu kulishughulikia litakapoamriwa basi tutawajulisha," Ahmed Ally.