Kiungo Mzambia anayekipiga Simba SC, Clatos Chota Chama, ameendelea kujikita kileleni kuwa kinara wa kutoa pasi za mwisho (asist) kwenye Ligi Kuu ya NBC.
Chama ambaye Januari 18, 2023 aliitumikia klabu yake kwa takriban dakika 30 kabla ya kufanyiwa sub na nafasi yake kuchukuliwa na Pape Osman Sakho, kwenye dakika hizo chache alizocheza, tayari alitoa asist kwa Saido Ntabanzokinza ambaye alifunga goli la kwanza dhidi ya Mbeya City.
Kwenye mechi hiyo ambayo Simba ilikuwa ikikamilisha raundi ya 20, Chama alifikisha asist ya 12 na kuwa kinara akifuatiwa na Ayoub Lwanga mwenye asist 7, Saido (7), Sixtus Sabilo (6). Deus Kaseke (5), Mohamed Hussein (5) na Yassini (5).