Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama awagawa mabosi Simba, mwamba agoma kusaini

Realclatouschama Chama awagawa mabosi Simba, mwamba agoma kusaini

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kweli bado hakijaeleweka kiungo mshambuliaji raia wa Zambia, Clatous Chota Chama bado hajamwaga saini ya kuendelea kusalia katika viunga vya wekundu wa msimbazi baada ya mabosi wa Simba kushindwa kumtekelezea mahitaji aliyowasilisha mezani ili asalie kikosini.

Ipo hivi utata umeibuka ni baada ya mabosi wa Simba kugomea kumuongezea ada ya usajili (Sign on Fee) ambayo kiungo huyo alikuwa anaitaka ili asaini mkataba wa kuendelea kusalia katika timu hiyo.

Simba ni kama imeingia nyongo na Chama ambapo baadhi ya mabosi ndani ya klabu hiyo wakiona Mzambia huyo bado anahitajika, huku kundi lingine lenye nguvu likiona ni bora watengeneze timu mpya itakayokuwa bila ya mchezaji huyo.

Hatua ya Pili ambayo Chama na Simba inabishana ni juu ya Mshahara ambao anautaka ambao ni zaidi na ule anaolipwa sasa winga Luis Miquissone, habari kutoka ndani ya SImba zinasema kuwa mabosi wa Simba na Chama wameshindwa kuafikiana  kwenye Dau hilo la mshahara kwani mzambia huyo ametaka kulipwa Dola 20,000 (Tsh 52 Milioni).

Kwasasa inadaiwa Luis Miquisson ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza au kupata nafasi ya kutumika mara kwa mara kikosini analipwa Simba zaidi ya Dola 17,000 (Tsh 44Milion) kwa mwezi mshahara ambao Chama ametaka zaidi ya kiwango hicho ili asaini mkataba mpya na mabosi wa Simba wanaona ni vigumu kumkubalia.

Hatua ya mwisho kwa Simba ni kama Kundi linalotaka Chama aachwe linaelekea kushinda kwa vile ndio wanaotoa uamuzi mkubwa kwenye Bajeti ya klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live