Kiungo wa Simba, Clatous Chama aliyeungana na wenzake kambini hivi majuzi amekiri kwa sasa Simba ina kikosi kizuri na chenye ushindani na anaweza kusema wazi msimu ujao wapinzani watapata tabu sana.
"Tupo kwenye maandalizi ya msimu mpya kuna wachezaji wengi wapya tunapambana kuhakikisha tunatengeneza muunganiko mzuri ambao utakuwa na tija ndani ya timu msimu ujao," alisema Chama aliyemaliza msimu uliopita akifunga mabao matatu na kuasisti mara 14.
"Lengo ni kuhakikisha tunamaliza msimu tukiwa na mataji muhimu ambayo yataturejesha kwenye ushindani hasa kimataifa ambapo tunatamani kuvuka hatua ambazo tayari tumezipiga kwa misimu minne mfululizo hilo linawezekana tukiendeleza juhudi zetu na kuwa wamoja," Chama aliongeza.
Chama alisema wachezaji waliosajiliwa Simba wote ni wazuri na anaamini watakuwa chachu ya wao kuwa bora zaidi ya msimu uliopita ambao hawakufanikiwa kutwaa taji hata moja.
ONANA MTU NA NUSU
Kiungo mshambuliaji huyo, hakusita kumwagia sifa mshambuliaji mpya Willy Onana aliyesema ni moja ya sajili bora zilizofanyika Simba, huku akitamba msimu huu yatafungwa mabao mengi.
"Sio sahihi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja kama nilivyozungumza hapo mwanzo kuwa usajili uliofanywa ni wa kuwapongeza viongozi na ni kazi kwetu kuwafanyia kilocho bora," alisema Chama na kuongeza;
"Onana kama unavyotaka nimzungumzie ni mchezaji mzuri anajua kukaa kwenye nmafasi atafunga sana msimu ujao ameonyesha kuwa na kitu kwenye mguu wake anapenda kufunga Simba itafunga mabao mengi sana msimu ujao japo ni kawaida kutokana na safu yetu kujua kutimia nafasi."
Akimzungumzia kurudi kwa Luis alisema amefurahi na anaamini atafanya mambo makubwa huku akikiri kuwa alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara kuhusu mpira anaamini kurejea kwake ataweza kufanya mambo makubwa.
"Nimefurahi kukutana tena na Luis nilikuwa nikiwasiliana naye mara nyingi nalaikuwa anatamani kurudi Simba kutokana na kutamani kupata nafasi ya kucheza ili kuendeleza kipaji chake sasa naamini atakuwa imara na atafanya vizuri.