Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama atambulishwa kwenye jezi ya Wananchi

SASACHAMA Chama atambulishwa kwenye jezi ya Wananchi

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Mwamba wa Lusaka, Chama Clatous akiwa na jezi ya timu hiyo.

Awali Chama alitambulishwa akiwa anasaini mkataba tena amevalia koti bila jezi ya Yanga jambo lililozua maswali mengi kwa mashabiki, wachambuzi wa soka, na wadau wa soka nchini.



"Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama raia wa Zambia ni mchezaji halali wa Young Africans SC.

"Chama ambaye kiwango chake kimekuwa kivutio machoni mwa watazamaji amejiunga na Young Africans akitokea kwa watani zetu wa jadi hapa nchini.

"Kiungo huyo ambaye ana uzoefu na soka la Tanzania, alianza kuonesha uwezo wake hapa nchini mwaka 2018 alipotua kwa mara ya kwanza akitokea Lusaka Dynamos ya kwao Zambia.

"Ujio wa Chama katika kikosi chetu unaongeza wigo mpana katika eneo la kiungo cha ushambuliaji.

"Rekodi za Chama katika Ligi Kuu Tanzania Bara zinaonesha kwamba amecheza mechi 139 akifunga magoli 27 na asisti 54, huku michuano ya CAF katika misimu sita iliyopita akicheza mechi 44, amefunga magoli 15 na asisti 6.



"Haya ni maboresho ya kikosi chetu katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu ujao wa 2024-2025 tukiwa na malengo ya kutetea mataji yetu yote tuliyobeba msimu wa 2023-2024 ambayo ni Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank Federation huku pia tukihitaji kufanya vizuri zaidi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuishia robo fainali msimu uliopita.

"Chama anaungana na nyota wengine wapya ndani ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao ambao ni Prince Dube, Chadrack Boka, Khumeiny Aboubakar na Aziz Andambwile," imesema taarifa ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live