Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama amsapraizi Mkude

Mkude X Allende Chama amsapraizi Mkude

Mon, 1 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubora aliouonyesha kiungo wa Yanga, Jonas Mkude kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns umewaibua mastaa kibao huku kiungo wa Simba, Clatous Chama akimuahidi zawadi mwisho wa msimu.

Mkude alicheza eneo la kiungo mkabaji akichukua nafasi ya Khalid Aucho ambaye yupo nje ya uwanja kwa muda akiuguza jeraha la goti alilolipata kwenye mchezo wa makundi dhidi ya Al Ahly ugenini timu yake ikikubali kichapo cha bao 1-0.

Baada ya mchezo wa juzi mastaa mbalimbali wanaocheza Ligi Kuu Bara kutoka timu tofauti wametoa maoni yao kwenye ukurasa wa Instagram wa Mkude wakimpongeza kwa kiwango alichoonyesha.

Kiungo wa Simba, Chama, alienda mbali zaidi kwa kumuahidi Mkude zawadi msimu huu utakapomalizika huku akimtaka ampe tiketi ya ndege waende wote Lusaka Zambia baada ya msimu kwisha.

"Mjomba 'angu Mkude wewe hatari, baada ya msimu kuisha njoo uchukue zawadi yako au unataka tiketi nikupeleke Lusaka kidogo mechi nzuri," ameandika Chama.

Kiungo wa Yanga, Aucho ameandika "Hongera kwa mchezo mzuri umefanya kazi nzuri kiungo kila jema liwe upande wako."

Salum Abubakar 'Sure Boy' aliandika: "Ilikuwa siku njema kwako ulifanya kilicho bora daima mambo yaendelee kuwa bora, daima mbele nyuma mwiko."

Kiungo wa Singida Fountain Gate, Aziz Andabwile aliandika: "Kiungo fundi kwenye majukumu sahihi ulifanya kazi uliyoagizwa hongera kaka mkubwa."

Ramadhan Chombo 'Redondo' aliandika, "kiungo Nungunungu mzito ulikuwa bora sana kazi iendelee."

Mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda aliandika "Nungunungu ulikuwa bora sana bado dakika nyingine 90 haachwi mtu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live