Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama ameshuka kiwango, Aziz Ki ni bora zaidi - Kamwe

Chama Ameshuka Kiwango, Aziz Ki Ni Bora Zaidi   Kamwe Chama ameshuka kiwango, Aziz Ki ni bora zaidi - Kamwe

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clotous Chama, ameshuka kiwango na huwezi kumfananisha na Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Aziz Ki.

Kamwe ameyasema hayo alipoulizwa kuhusu uwezo mtazamo wake juu ya viungo hao ambao wanaonekana kufanya vizuri katika ligi ya NBC.

"Season hii hakuna namna unaweza kumuweka Chama mbele ya Aziz Ki, achana na historia, tunaongelea current ni kwamba Aziz Ki ni bora kuliko Chama. Wanasema class is permanent form is temporary hivyo Chama ana class lakini form imeshuka.

"Aziz Ki ana class na yupo kwenye form nzuri, namba zake msimu huu zinaongea na hiyo ni fact zinaongea," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live