Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama aingia kwenye mfumo, Mbrazili afichua siri

FoMUijBWIAASDbZ Chama aingia kwenye mfumo, Mbrazili afichua siri

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Uliona kiwango kipya cha kiungo fundi kutoka Zambia, Clatous Chama kwenye mechi ya Simba na Singida Big Stars? Achana na ule ufundi wake miguuni, lakini kasi aliyokuwa nayo katika kuisukuma timu na hata kufanya maamuzi. Sasa sikia hii!

Simba imeanza kutembea katika mifumo ya kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' anavyotaka soka flani la pasi nyingi za haraka na kasi kuelekea lango la wapinzani, ambayo nusura imtibulie Chama katika mechi ya kwanza kwa Mbrazili huyo dhidi ya Mbeya City na kumchomoa dakika ya 33 tu.

Kisha kiungo huyo aliamua kuzira kuambatana na timu kwenda Dodoma kwenye mechi ya dhidi ya Dodoma Jiji, lakini baada ya Mbrazili kurudi kutoka kwao alikaa chini na kiungo huyo na kumpa darasa na jamaa ghafla kabadilika na kuupiga mpira na kuingia kwenye mfumo wa Robertinho.

Katika mechi ya juzi ambayo Simba ilishinda mabao 2-1, Chama alionekana mpya kabisa kwa kuongeza kasi kuelekea katika lango la wapinzani lakini bado akibali na ubora wake kutengeneza pasi za mwisho za mabao sambamba ufundi wake unaowakuna mashabiki wa klabu hiyo.

Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars kuonyesha kwamba bado Chama yule yule Mzambia huyo alitoa pasi mbili za mabao wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-1 huku mwishoni ikiupiga mwingi mpaka firimbi ya mwisho ya mwamuzi.

MSIKIE MBRAZILI

Kocha Robertinho alisema baada ya mchezo wa City kupita alikaa chini na Chama kumueleza vile ambavyo anahitaji kumuona akicheza muda wote anapokuwa uwanjani.

Robertinho alisema Chama ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na mtulivu haswa anapokuwa na mpira mguuni kwake kwa maana hiyo alimueleza anataka kumuona akiongeza kasi na kushambulia kwa haraka.

Alisema baada ya kuongea nae kwenye mazoezi ya kujiandaa mchezo wa Kombe la Shirikisho (ASFC) na ule wa Ligi Kuu Bara alikuwa akimpatia mazoezi mbalimbali kwa vitendo ili kwenda kuvifanyia kazi.

"Kutokana na uelewa mkubwa wa Chama aliyokuwa nao wala halikuchukua muda hili kwenye mchezo dhidi ya Singida nadhani kila mmoja aliona mabadiliko makubwa aliyokuwa nayo," alisema Robertinho na kuongeza;

"Chama alipokuwa na mpira utulivu wake ulikuwepo kwa kupiga pasi nzuri, kuanzisha mashambulizi, kuwasumbua wachezaji wa timu pinzani ila aliongezeka uharaka kwenye matukio yote hayo. Kama ulimuangalia vizuri mpira ulipopotea alirudi haraka chini kuutafuta, alipora mipira na baada ya kuupata alikuwa na uharaka kwenye kushambulia.

"Chama alitoa pasi mbili za mabao na ubora wake ulikuwa mkubwa kutokana na mabadiliko ya uchezaji wake na naimani huo ndio utakuwa uchezaji wake wa sasa hata katika michezo inayofuata," alisema Roberthino ambaye tangu akabidhiwe timu haijapoteza kwenye mechi za mshindano akishinda tatu za Ligi Kuu na moja ya ASFC.

"Hata baada ya mechi kuisha niliongea nae na alionekana kuwa mwenye furaha huku binafsi nikiamini Chama atakwenda kuwa bora zaidi kwenye aina hii ya uchezaji wa sasa niliyombadilisha," aliongeza Robertinho aliyeiongoza timu jana jioni kuvaana na Al Hilal katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Chanzo: Mwanaspoti