Oktoba 20, Clatous Chama atakuwa na kibarua dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye mechi ya uzinduzi ya mashindano ya Afrika Football League katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, lakini kabla ya hapo atavaana na Wamisri akiwa na kikosi cha timu yataifa lake ya Zambia 'Chipolopolo'.
Hiyo ni kufuatia kitendo cha kocha Avram Grant kumjumuisha katika kikosi cha Chipolopolo kitakachocheza mchezo huo wa kujipima nguvu dhidi ya Misri, Oktoba 12 na siku tano baadaye kuumana na Uganda.
Kiwango bora cha Chama ndani ya Simba msimu huu kimeendelea kumshawishi kocha Grant kumjumuisha kikosini kama alivyofanya pindi Zambia ilipokuwa inasaka tiketi ya kushiriki Afcon 2023, lakini kocha huyo hajamuita nyota wa Yanga, Kennedy Musonda.
Grant ameita kundi la nyota 25 kwa ajili ya mechi hizo mbili za kirafiki, ambapo nyota 11 wanacheza soka nyumbani huku 14 wakicheza soka la kulipwa nje ya Zambia.
Nyota wa zamani wa Simba anayeitumikia Shekhukhune ya Afrika Kusini, Rally Bwalya naye amejumuishwa katika kikosi hicho cha Chipolopolo ambacho hakitakuwa na Lameck Banda wa Lecce ya Italia na Frankie Musonda wa AYR United ya Scotland ambao ni majeruhi.
Kikosi hicho cha Zambia kinaundwa na makipa Francis Mwansa (Green Buffaloes), Charles Kalumba (Red Arrows), Victor Chabu (Nchanga Rangers) wakati mabeki ni Benedict Chepeshi (Red Arrows), Zephaniah Phiri (Prison Leopards), Stoppila Sunzu (Jinan Xingzhou), Gift Mphande (Hapoel Lishon Lezion), Luka Banda (Napsa Stars), Dominic Chanda (Power Dynamos), Roderick Kabwe (Zakho Sports Club), John Chishimba (Zesco United), Golden Mafwenta (MFK Vyskov),
Viungo walioitwa ni Kelvin Kapumbu, Kelvin Kampamba (Zesco United), Kings Kangwa (Crzena Zvezda), Clatous Chama (Simb), Emmanuel Banda (Rijeka) na Rally Bwalya (Sekhukhune).
Wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji ni Lubambo Musonda (Silkeborg IF), Edward Chilufya (Hacken), Fashion Sakala (Club Al Fayha), Francisco Mwepu (Atletico Sanluqueno), Evans Kangwa (Quingdao Hainiu), Patson Daka (Leicester City) na Moyela Libamba (Forest Rangers)