Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama aahidi pointi tatu dhidi ya Kagera

Tripple C Chama aahidi pointi tatu dhidi ya Kagera

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, amesema wanamshukuru Mungu wamesafiri na kufika salama mkoani Kagera tayari kwa ajili ya kuwavaa, Kagera Sugar.

Chama amesema wanafahamu kwamba mara ya mwisho walipoteza kwa goli moja kwenye uwanja wa Kagera, Kaitaba na hilo linawapa morari ya kuongeza nguvu zaidi katika mchezo wa leo Desemba 21, 2022.

"Tunafahamu tulipoteza hapa Kaitaba, hii inatupa morari ya kuongeza nguvu ili mwisho wa siku tuweze kupata alama tatu muhimu hii hapo kesho (leo)," alisema Chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live